Kagame na Tshisekedi kukutanishwa uso kwa uso Desemba 15
Eric Buyanza
December 3, 2024
Share :
Mkutano wa kuendelea na mchakato wa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unatarajiwa kutafanyika Desemba 15 kwenye jiji la Luanda nchini Angola.
Mkutano huo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kutafuta suluhu ya kudumu kutokana na mzozo unaoendelea Mashariki mwa Kongo ambapo Rais wa Angola Joao Lourenço ameteuliwa na Umoja wa Afrika kama mpatanishi.
Mkutano huu utawaleta pamoja Marais Félix Tshisekedi wa DRC, Paul Kagame wa Rwanda, pamoja na mwenyeji wao Joao Lourenço wa Angola, ili kuharakisha juhudi za kuleta utulivu katika eneo hilo.