pmbet

Kahn awataja Klopp na Deschamps kuwa wanafaa kuinoa Madrid

Eric Buyanza

April 18, 2026
Share :

Gwiji wa Bayern Munich, Oliver Kahn, amewataja makocha wawili ambao wanaweza kukinoa kikosi cha Real Madrid ikiwa wataamua kuachana na Alvaro Arbeloa.

 

Arbeloa amekuwa chini ya shinikizo baada ya Real Madrid kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya UEFA Champions mikononi mwa Bayern Munich siku ya Jumatano.
 

Kwa sasa, Real Madrid wanatazamiwa kumaliza msimu bila taji lolote, na kwa sababu hiyo, wababe hao wa LaLiga wanaweza kuchukua nafasi ya Arbeloa mwishoni mwa msimu huu.

 

Alipoulizwa na Sky Sport kuhusu meneja gani anaweza kuwa kocha mpya wa Real Madrid katika siku za usoni, Kahn alimtaja kocha mkuu wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp na kocha mkuu wa sasa wa Ufaransa Didier Deschamps.
 

"Nafikiri mwanaume mwenye uzoefu kama Didier Deschamps anaweza kuachia ngazi baada ya Kombe la Dunia na kisha kuchukua Real Madrid," Kahn alisema.

 

"Pia ningeweza kumfikiria kwa urahisi Jurgen Klopp ambaye ameweka wazi kuwa bado anafurahia kazi yake ya sasa.”

 

"Lakini mambo yanaweza kubadilika haraka katika soka. Real Madrid inapopiga simu, kwa kawaida huwezi kukataa" alimalizia Gwiji huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet