pmbet

Kaka wa Amrabat asimulia namna Casemiro alivyojivunja fainali ya FA

Sisti Herman

June 4, 2024
Share :

Kaka wa kiungo mkabaji wa Mnchester United, Sofiane Amrabat, Nordine Amrabat akiwa kwenye kituo kioja cha televisheni cha Ziggo Sports amesema kuwa kiungo mkabaji wa Manchester United raia wa Brazil Casemiro hakuwa na majeraha yaliyomfanya kukosa mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester City kama ilivyoelezwa bali alisingizia kuumia ilhali hakuumia.

"Casemiro hakuwa na majeraha siku ya ainali ya FA, alivyoona hakuwa kwenye mipango ya kuanza akajishtukia mwenyewe na kukaa jukwaani akisngizia kuwa hayupo fiti" alisema Nordine.

Sofiane amesema hayo akisimulia namna kiwango cha mdogo wake Sofiane Amrabat kupanda maradufu kwenye mwezi wa mwisho United kiasi cha Casemiro kusugua benchi huku wakihanikiza klabu hiyo impe mdogo wake mkataba mpya.

Kwenye mchezo huo Man Utd ilibeba taji kwa kuwafunga City 2-1.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet