Kaka wa Michael Jackson, ashtakiwa kwa ubakaji
Eric Buyanza
December 30, 2023
Share :
Jermaine Jackson, mmoja wa kaka mkubwa wa marehemu Michael Jackson na mwanachama mwanzilishi wa kundi la 'Jackson 5', anashtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono.
Katika malalamiko yaliyowasilishwa Jumatano wiki hii jijini Los Angeles, Rita Barrett anasema mwanamuziki huyo alimbaka nyumbani kwake mwaka 1988.
Katika kesi ya madai iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Los Angeles California, Rita anamshtaki Bw. Jackson kwa unyanyasaji wa kingono tukio ambalo anasema lilitokea nyumbani kwake Los Angeles.
Bi. Barrett anasema kwamba Bw. Jackson aliingia kwa nguvu nyumbani kwake na kumshambulia, na kumsababishia majeraha makali ya kihisia, kimwili, kiakili, fedheha, aibu, hasara ya kiuchumi pamoja na mfadhaiko wa kudumu wa kihisia.
Bw. Jackson mwenye umri wa miaka 69 hivi sasa, bado hajajibu tuhuma hizo.