Kale kamsemo kanakufa lini ?...! Marioo avunja benki kisa birthday ya Paula.
Joyce Shedrack
July 18, 2024
Share :
Mpenzi wa msanii wa bongofleva ambaye ni mtoto wa muigizaji Kajala Frida, Paula Kajala amechapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram inayoonyesha jinsi sherehe yake ya birthday ilivyokuwa akionekana kumshukuru Mungu kwa aina ya mwanaume aliyempata.
Paula ambaye ni mzazi mwenzake na Marioo siku mbili zilizopita alikuwa anasherekea kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa akitimiza miaka 22.
Marioo amemtungia mpenzi wake ngoma aliyoiachilia siku ya sherehe hiyo ya kumbukumbu ya kuzaliwa.