“Kama hajatoa barua wanatembea tu...hiyo inaitwa kuchezeana” - Mama Dangote
Eric Buyanza
January 13, 2024
Share :
Diamond na Zuchu wamekuwa kwenye mahusiano yenye utata ambayo yamewaacha wengi wakijiuliza bila kujua mahusiano yao yanahusiana na nini?
Katika mahojiano latest kabisa, mama Diamond (Mama Dangote) anasema kuwa mwanae hajawahi kumtambulisha Zuchu kuwa mke mtarajiwa.
Kwa maneno yake:
"Kwa sasa hivi mimi najua Naseeb hajanitambulisha mke wala mchumba, unajua mchumba unatambulishwa mama unakua ushatoa barua, ushaona? Bwana mimi mtu fulani nataka nimuoe barua tunatuma tunaenda kumuona mchumba tunajua huyu mtu atamuoa"
"Lakini kama hajatoa barua wanatembea tu...hiyo inaitwa kuchezeana...ndio hivyo, mimi hajawahi kuniletea Zuchu anataka kumuoa, mimi Zuchu kwanza navyojua ni msanii wake...sasa hayo ya kusema kama Zuchu mchumba wake sijui...kwasababu mimi sijapeleke mahari kwa kina Zuchu wala barua" anasema Mama Dangote