Kama hatushindi siwezi kuwa na furaha - Benchikah
Eric Buyanza
December 4, 2023
Share :
Baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere wakitokea Botswana, safari ya zaidi ya saa 4, kocha wa Simba, Abdelhack Benchikah amefunguka mengi akitoa tathmini yake fupi baada ya mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Jwaneng' Galaxy kwa waandishi waliofika uwanja wa ndege akiwepo mwandishi wa habari hii.
"Tulikuwa na uwezekano wa kushinda na kufunga mabao mengi lakini ndio mpira, nina furaha kwasababu wachezaji wangu walijitoa, tumechukua alama moja, tuna mambo mengi ya kufanyia kazi na kubadilisha na kuweka mazingira kuwa mazuri kwetu, kwasababu kama hatushindi siwezi kuwa na furaha" alisema Benchikah ikiwa ni mchezo wake wa kwanza.
Simba imepata hatisafi (cleansheet) kwenye mchezo wa kwanza wa Benchikah baada ya kuwa na rekodi mbaya ya kuruhusu bao kwenye michezo 10 mfululizo huku kwenye mechizo 10 iliyopita ikiruhusu mabao 14, mwanzo mzuri waujenzi wa kikosi kwa Benchikah, mchezo ukimalizika kwa sare ya 1-1 ugenini.