pmbet

Kama kawaida yake kocha wa Yanga amezua gumzo tena huko Malawi.

Joyce Shedrack

September 4, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Yanga Manqoba Mngqthi amezungumza kuelekea mchezo wao wa siku ya kesho dhidi ya  Gaborone United huku akiwataja baadhi ya wachezaji wa timu pinzani ambao watakosekana kwenye mchezo huo.
 

“Tunakwenda kucheza mchezo ambao kwa kweli ni mgumu. Tunacheza michezo miwili mwishoni mwa wiki hii lakini kwa bahati nzuri tumepata siku chache za kujiandaa na kikosi”

"Kwanza, lazima nimpe heshima Kocha Sean Connor. Nafikiri amefanya kazi kubwa sana na timu hii. Tangu alipoanza kuifundisha nimekuwa nikifuatilia kinachoendelea na naamini ameibadilisha na kuwa timu nzuri sana" 

 

"Kwa upande wa ulinzi ni timu imara. Hairuhusu mabao mengi na pia ni hatari sana inapofanya mashambulizi ya kushtukiza pamoja na mipira iliyokufa (set pieces).

"Sijui kutokuwepo kwa Mothusi Johnson na Mpho Kgwaswane kutakuwa na athari gani kwa timu yao kwa sababu wote walikuwa wachezaji muhimu sana. Hata hivyo bado wana kipa mwenye uzoefu pamoja na wafungaji wawili wazuri na kipa kutoka Namibia. Pia wana beki wa kulia mwenye uwezo mkubwa" @manqoba.mngqithi
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet