pmbet

Kama mshahara wa mke wangu haupitii kwangu, basi aache kazi

Eric Buyanza

February 10, 2024
Share :

Jamaa mmoja huko Nigeria amemuamuru mke wake kuacha kazi baada ya bosi wa mwanamke huyo kumtaka afungue account yake ya benki itakayotumika kupitishia mshahara wake moja kwa moja badala ya kupitishia kwenye akaunti ya mume wake.
 

Mwanamke huyo alikuwa akitumia akaunti ya mume wake kupitishia mshahara wake jambo ambalo lilikuwa likimkera bosi huyo.
 

Kwa mujibu wa Bosi wa mwanamke huyo, anasema yeye hulipa mshahara wa mke kwenye akaunti ya mume na hivyo anaona kabisa kuwa mke anakosa umiliki halali wa pesa zake na ndio maana akamshauri afungue akaunti binafsi.
 

Muajiri huyo aliyeajiri idadi kubwa ya wanawake aliamua kusaidia kwa kuwapa wanawake udhibiti wa moja kwa moja wa pesa zao. Hata hivyo, jitihada zake za kumsaidia mke huyo ziliambulia patupu.
 

Bosi huyo aliandika kupitia mtandao wake wa kijamii "Nilimshauri msafishaji wangu aende kurekebisha masuala yake ya akaunti ili niache kutuma mishahara yake kwenye akaunti ya mumewe ili aweke akiba na kudhibiti pesa zake alizochuma kwa bidii........cha ajabu mume alimwambia mke asirudi tena"
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet