pmbet

"Kama mwili wangu utaruhusu nitashiriki EURO 2028"-Ronaldo.

Joyce Shedrack

September 24, 2026
Share :

Nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo ameweka wazi uwezekano wa kuendelea kuichezea timu ya taifa hadi michuano ya Euro 2028, licha ya kukiri kuwa msimu huu unaweza kuwa wa mwisho kwake katika soka la ushindani.

Cristiano Ronaldo Portugal Nations League Trophy Editorial Stock Photo -  Stock Image | Shutterstock Editorial

Ronaldo amesema hataki kufanya uamuzi wa haraka kuhusu mustakabali wake, akisisitiza kuwa afya ya mwili na hali yake ya kiakili vitakuwa miongoni mwa mambo yatakayoamua kama ataendelea kucheza.

 

“Je, huu utakuwa msimu wangu wa mwisho? Labda, sijui. Huu unaweza kuwa msimu wangu wa mwisho, lakini hatujui. Tutaona,”

 

“Euro 2028? Tutaona. Ninaishi maisha yangu siku baada ya siku.”

“Kama mwili wangu utaniruhusu, akili yangu nayo ikiwa tayari, na kama bado nitakuwa katika hali nzuri, basi sijui. Sijui kitakachotokea baadaye,” 

 

Ronaldo amesema kipaumbele chake ni kusaidia Ureno katika Ligi ya Mataifa ya Ulaya(Nations League) na kuendelea na harakati zake za kufikisha jumla ya mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet