Kama ningekuwa Man U, ningemchukua Fernandes kutoka West Ham - Owen
Eric Buyanza
June 13, 2026
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Michael Owen, amemshauri Michael Carrick kumsajili Mateus Fernandes wa West Ham kuchukua nafasi ya Casemiro.
Ikumbukwe kuwa Casemiro tayari ameondoka Man United baada ya kumalizika kwa msimu wa 2025/26.
Owen anaamini Fernandes ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kufanya kazi nzuri kwa Mashetani Wekundu.
Akiongea na Metro Owen alisema:
"Binafsi kama ningekuwa Michael Carrick, kama ningekuwa Manchester United, ningemchukua Fernandes kutoka West Ham. Nadhani ni mzuri sana. Nadhani ndiye kile wanachohitaji." alisema Owen alipoongea na Metro.





