Kama siyo U.S.A, Israel isingekuwepo - Trump
Sisti Herman
November 9, 2026
Share :

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel isingekuwepo bila msaada wa Marekani, akidai nchi yake imekuwa na mchango mkubwa katika kuilinda Israel dhidi ya vitisho vya kiusalama.
Katika mahojiano jana Novemba 8, 2026 na shirika la habari la CBS, Trump alitaja shambulio la Marekani dhidi ya vituo vitatu vya nyuklia vya Iran lililofanywa kwa kutumia ndege za kivita aina ya B-2, akisema hatua hiyo ilikuwa muhimu katika kuilinda Israel.
"Pasipo sisi, Israel isingekuwepo. Naomba niwaambie kama si Donald Trump, Israel isingekuwepo, kwa sababu zaidi ya mwaka mmoja uliopita tulituma ndege zetu nzuri za kivita aina ya B-2 na kushambulia maeneo yote matatu," alisema.
Trump alitoa kauli hiyo alipoulizwa kuhusu gharama za uwepo wa kijeshi wa Marekani Mashariki ya Kati, akisisitiza nchi ambazo zimenufaika na ulinzi wa Marekani zinapaswa kurejesha gharama zote zilizotumika katika operesheni za kijeshi.
Alisema nchi hizo zinapaswa kutambua mchango wa Marekani, akidai zisingeweza kuendelea kuwepo bila msaada wa kijeshi wa nchi hiyo.
Katika mahojiano hayo, Trump pia alitetea mashambulizi dhidi ya Iran, akisema manufaa yake yataonekana baadaye na kwamba angehukumiwa vikali na historia iwapo Iran ingepata silaha za nyuklia wakati akiwa madarakani.





