Kamala Harris ajitoa mbio za Ugavana 2026 na Urais 2028.
Joyce Shedrack
July 31, 2025
Share :
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Ameweka wazi kuwa hatagombea tena nafasi ya Urais kwenye uchaguzi ujao mwaka 2028 wala Ugavana wa California mwaka 2026 baada ya kuibuka tetesi kuwa anaitaka nafasi hiyo.

Akizungumza siku ya jana kupitia mahojiano aliyoyafanya mpinzani huyo wa Donald Trump katika uchaguzi mkuu uliopita wa Taifa hilo Kamala amesema uongozi wake hautotokana kwa kuchaguliwa tena.
“Ninalipenda Jimbo langu na watu wake ni nyumbani kwangu lakini baada ya kujitafakari nimefanya maamuzi ya kutokugombea nafasi ya Ugavana kwa sasa uongozi wangu na huduma yangu kwa umma haitakuwa katika nafasi ya kuchaguliwa,” Amesema Kamala Harris.





