pmbet

Kamala Harris ajitosa kushindana na Trump.

Joyce Shedrack

July 22, 2024
Share :

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris (59) ametangaza nia yake ya kugombea Urais wa Nchi hiyo akiahidi kufuata nyayo za Rais Joe Biden na kushinda uteuzi wa Chama cha Democratic baada ya Biden kujiondoa kwenye kinyang’anyiro.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia kampeni ya Biden-Harris, Harris ametoa shukrani kwa uidhinishaji wa Rais Biden. 

“Nimejivunia kuidhinishwa na Rais na nia yangu ni kupata na kushinda uteuzi huu,tuna siku 107 kabla ya Siku ya Uchaguzi pamoja tutapigana na kwa pamoja, tutashinda,” amesema Kamala

Ikumbukwe, baada ya Rais wa Nchi hiyo Biden kutangaza kuachia nafasi hiyo aliweka wazi kumuunga mkono Makamu wake ili kugombea Urais kupitia Chama chake cha Democratic kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 2024.
 

Biden alisema  katika chapisho lingine kwenye mtandao X.
“Leo nataka kutoa uungwaji mkono wangu kamili na uidhinishaji kwa Kamala kuwa mteule wa chama chetu mwaka huu “Democrats - ni wakati wa kukusanyika na kumpiga Trump.”.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet