Kambi ya Matibabu Arusha yageuka faraja kwa wananchi.
Eric Buyanza
June 26, 2024
Share :
Wananchi Jijini Arusha wameishukuru Serikali ya Mkoa wa Arusha ikiongozwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda kwa kuandaa Kambi ya madaktari bingwa inayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Wananchi hao wameonesha kufurahishwa na huduma za matibabu yanayoendelea kwenye Kambi hiyo ya matibabu, wakikiri uwepo wa Madaktari bingwa kutoka kwenye Hospitali na Taasisi za Matibabu zenye kuheshimika kitaifa na Kimataifa.
Aidha, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya nchini Tanzania kwa kuwezesha kambi hiyo na kutoa huduma za vipimo, matibabu pamoja na dawa ikiwemo pia vifaa tiba mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa leo ni siku ya tatu ya Kliniki ya Madaktari Bingwa iliyoanza siku ya Jumatatu Juni 24 yenye lengo la kutoa huduma za matibabu bure kwa wakazi wa Jiji la Arusha itakayofanyika kwa siku saba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.