pmbet

Kamevimba Bichwa...! JJ Gabriel ataka kuondoka Man United

Sisti Herman

September 16, 2026
Share :

 

Kinda mwenye Kipaji cha kipekee wa Manchester United, JJ Gabriel, mwenye umri wa miaka 15, ameripotiwa kuishangaza klabu hiyo baada ya kuomba usajili wake ufutwe ili aondoke mara moja.

Kinda huyo, ambaye amekuwa akitazamwa kama mmoja wa wachezaji wenye mustakabali mkubwa zaidi katika akademia ya miamba hiyo ya Old Trafford, amewasilisha maombi rasmi ya kutaka kuachana na mashetani hao wekundu.

Taarifa kutoka vyanzo vya karibu na klabu hiyo zinasema kuwa uamuzi huo umewashtua viongozi na makocha wa timu za vijana, ambao walikuwa na mipango mikubwa na chipukizi huyo.

JJ Gabriel amekuwa akivutia macho ya wapenzi wa soka kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira na kufunga mabao, hatua iliyomfanya kulinganishwa na mastaa wakubwa duniani tangu akiwa na umri mdogo.

Hadi sasa, sababu za msingi zilizomfanya mchezaji huyo kuomba kuondoka kwa ghafla hazijawekwa wazi na upande wa mchezaji au klabu yenyewe.

Uongozi wa Manchester United bado haujatoa tamko rasmi kuhusu hatua utakayochukua, lakini wadadisi wa mambo wanasema klabu hiyo itajaribu kufanya kila liwezekanalo kuzungumza na familia ya mchezaji huyo ili kubadili msimamo wake kabla ya kufikia maamuzi ya mwisho.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet