Kampeni ya 'Visit Rwanda' yawa wadhamini wakuu wa Aston Villa
Sisti Herman
July 14, 2026
Share :

Mamlaka ya Utalii nchini Rwanda, Visit Rwanda, imetangaza ushirikiano mpya na klabu ya Aston Villa ya Ligi Kuu England, katika mkataba ambao utaiwezesha nembo ya kampeni hiyo kuonekana mbele ya jezi za klabu kuanzia msimu wa 2026/27
Makubaliano hayo yanatajwa kuwa miongoni mwa mikataba mikubwa zaidi ya kibiashara katika historia ya Aston Villa.
Hatua hiyo imekuja baada ya ushirikiano wa miaka minane kati ya Visit Rwanda na Arsenal kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
Rwanda imeendelea kutumia ushirikiano na vilabu vikubwa vya Kimataifa kuitangaza sekta yake ya Utalii na uwekezaji.





