Kampeni za uchaguzi mkuu kuanza kutimua vumbi Agosti 28.
Joyce Shedrack
July 26, 2025
Share :
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia kwa Mwenyekiti wake Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema tarehe 09 hadi 27 Agosti, 2025 itakuwa ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea kwa kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
“Tarehe 14 hadi 27 Agosti 2025 itakuwa ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani, tarehe 27 Agosti 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani”, amesema Jaji Mwambegele.
Aidha tarehe 28 Agosti hadi 28 Oktoba 2025 itakuwa ni kipindi cha kampeni za Uchaguzi wa Tanzania Bara na tarehe 28 Agosti hadi 27 Oktoba 2025 itakuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi wa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema.
Ikumbukwe tarehe 29 Oktoba 2025 siku ya jumatano itakuwa ndiyo siku ya kupiga kupiga kura.