pmbet

Kampuni yatengeneza 'Kopo la kinywaji' linalojipooza lenyewe

Eric Buyanza

March 26, 2025
Share :

Kampuni moja nchini Uingereza imekuja na ubunifu wa kiteknolojia kwa kutengeneza kopo la kinywaji linalojipooza lenyewe ambalo wameliita(Cool Can) jambo litakaloifanya friji siku za mbeleni ionekane ni jambo la kizamani.

Kulingana na James Vyse, mwanzilishi wa kampuni hiyo, kinywaji kilichomo ndani ya kopo hilo (Cool Can) huchukua dakika 10 tu ili kufikia ubaridi unaopaswa na hudumu kwenye ubaridi huo kwa dakika takriban 45.

Kampuni hiyo imedai tayari iko kwenye mazungumzo na kampuni kubwa za vinywaji kama Coca-Cola na Red Bull kwa ajili kuwauzia teknolojia hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet