Kane aandika rekodi mpya Bundesliga
Sisti Herman
March 10, 2024
Share :
Mara baada ya jana kufunga mabao matatu (Hat-trick) kwenye mchezo wa ligi kuu Ujerumani kwenye ushindi wa 8-1 dhidi ya Mainz 05, mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uingereza Harry Kane akiwa na Bayern Munich msimu huu hadi sasa amefikisha;
- Mechi 34
- Magoli 36
- Asisti 10
Hiyo ni rekodi ya kipekee na ya haraka zaidi kuwahi kufikiwa huku kwenye Bundesliga pekee hadi sasa akiwa amecheza;
- - Mechi 25
- - Magoli 30
- - Asisti 8
Baada ya kufunga Hat-trick hiyo, Kane amefikisha hat-trick nne na amekuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo ndani ya msimu mmoja Bundesliga