pmbet

Kanisa katoliki laja na timu ya soka, lengo icheze Ligi Kuu

Sisti Herman

November 24, 2026
Share :

 

Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam limeanzisha timu yake ya soka ya St Joseph Sports Club ili iweze kushindana katika Ligi mbalimbali nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo ambaye pia ni Katibu Msaidizi wa Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jeremiah Ladislaus amesema malengo makuu ya timu hiyo ni kuibua na kutengeneza vipaji vya vijana pamoja na kuhakikisha timu inacheza michuano ya madaraja ya juu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika miaka ijayo.

"Muundo wa timu hii una mchanganuo wa vijana wenye umri chini ya miaka 20 na 17 pamoja na timu ya wakubwa na ya maveterani kwa wanaume na wanawake na lengo mama likiwa ni kuzalisha vipaji"alisema.

Alisema kwa kuanzia wana mchanganyiko wa wachezaji wenye umri tofauti wanaounda kikosi cha kwanza.

Alisema mchakato wa kupata timu hiyo ulianza mwezi Juni mwaka huu kwa kukusanya vijana mbalimbali na kuwafanyia mchujo na baada ya hapo walianza mazoezi kwa kipindi cha miezi mitatu na kisha mwishoni mwa Oktoba walianza kucheza mechi za kirafiki za kujipima ubavu ambazo wanaendelea nazo hadi sasa.

Kwa upande wake Afisa Habari wa timu hiyo Arone Mpanduka alisema tayari wamecheza mechi sita za kirafiki na wameshinda mechi tano na sare moja.

"Mechi za kirafiki tulizocheza zinatupa matumaini makubwa ya kufikia malengo yetu ambapo kwa sasa uongozi unafikiria kuanza kucheza Ligi ndogo ndogo za ushindani ili kuendelea kukipima kikosi.

Hata hivyo Mpanduka alisema licha ya harakati hizo, timu hiyo kwa sasa inasubiri kukamilika kwa mchakato rasmi wa usajili ambao mamlaka makuu yapo Baraza la Michezo la Taifa(BMT).

Alisema wapo mbioni kupeleka katiba ya klabu kwa uongozi wa BMT ili iweze kutambulika rasmi,ingawa hilo haliwazuii kuanza maandalizi ya uwanjani ili kujua mapema muelekeo wa timu.

Ikumbukwe mwishoni mwa miaka ya 90, Kanisa Katoliki liliwahi kuwa na timu ya soka iliyotikisa Ligi Kuu iliyofahamika kama Nazareti FC kutoka Njombe.

Timu hiyo iliyopewa jina la 'Watoto wa Baba Paroko' ndiyo chimbuko la wachezaji vinara ambao kwa sasa ni makocha kama vile Emmanuel Gabriel, Tigana Lukinja,George Mketo(kocha msaidizi JKT Tanzania
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet