Kanoute kuondoka Simba
Sisti Herman
May 5, 2024
Share :
Licha ya jitihada nyingi za Uongozi wa klabu ya Simba kuhitaji aendelee kubaki kwenye klabu hiyo, tetesi zinaeleza kuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Sadio Kanoute ameomba kuondoka mwishoni mwa msimu baada ya mkataba wake kutamatika.
Tetesi hizo zinadai kuwa uwezekano wa Kanoute kubaki Simba ni mdogo sana kwani mchezaji huyo raia wa Mali anahitaji changamoto mpya.