Kanye aja na viatu kama soksi, bila laki 5 hununui
Sisti Herman
December 29, 2023
Share :
Rapa na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani Kanye West ametangaza kuachia rasmi viatu vyake alivyovipa jila la ‘Yeezy pods’ venye thamani ya dola 200 ambayo ni zaidi ya Laki tano za Kitanzania.
YeezyPods ni aina ya viatu ambavyo muundo wake kama soksi huku urefu wake ukifikia magotini na kwasasa viatu hivyo vinapatikana kwa oda kupitia tovuti ya “Ye”.
Viatu hivyo vitakuwa ni toleo la kwanza kwa KanyeWest tangu kuvunja mkataba na kampuni ya Adidas miezi kadhaa iliyopita.