Kanye azuiwa kuingia Australia kisa wimbo wa kumsifu Adolph Hitler
Eric Buyanza
July 2, 2025
Share :
Rapa wa Marekani Kanye West amezuiwa kuingia Australia kutokana na wimbo wa kumtukuza kiongozi wa Nazi Adolf Hitler.
Waziri wa mambo ya ndani wa Australia Tony Burke alifichua kuwa idara yake ilikataa viza halali ya West baada ya kutoa wimbo wa Heil Hitler mapema mwezi wa Mei.
Wimbo wa West umeshutumiwa sana na umepigwa marufuku kwenye majukwaa mengi.
Rapa huyo mwenye utata, anayejulikana pia kama Ye, anajitambulisha kama Mnazi na anajulikana kwa misimamo yake ya chuki dhidi ya Wayahudi.