pmbet

Kanye kutomuunga mkono Trump

Sisti Herman

December 16, 2023
Share :

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Kanye West amesema kuwa hatoweza kumuunga mkono, Rais wa zamani Donald Trump mpaka amtoe gerezani Larry hoover na Young Thug (Jeff) ambaye yuko jela kwa kesi ya kukiuka sheria inayopambana na rushwa (RICO).

Kanye amemtaka Rais huyo wa zamani kumtoa jela Larry na kama itashindikana basi amtoe ‘rapa’ Young Thug (Jeff) jela.

Larry Hoover kwa sasa yuko katika gereza la ADX huko Florence Mjini Colorado, alihukumiwa kwenda jela zaidi ya miaka 150 baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya mwaka 1973, utakatishaji wa fedha na uuzaji wa dawa za kulevya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet