Kanye West aibwaga X zamani Twitter kisa maudhui ya Ngono aliyoyachapisha.
Joyce Shedrack
February 11, 2025
Share :
Rapa Kanye West amejiondoa tena kwenye mtandao wa X(zamani Twitter) baada ya kuchapisha maudhui mengi yaliyoibua taharuki kwenye mtandao huo siku za hivi karibuni mpaka pale alipoamua kufanya uamuzi huo jana.
Siku chache zilizopita Kanye West amekuwa akiongea vitu mbalimbali vilivyoibua hisia mbalimbali kwa wafuatiliaji wake huku wengi wakibaki na maswali kuwa anamepatwa na nini au ni muda wake wa kutrend umefika?.
Kubwa kuliko usiku wa jana aliacha watu midomo wazi baada ya bila aibu kubwa ya msanii huyo na kuweka maudhui ya ngono kwenye mtandao huo na baadae kuyafuta kabla hajafikia uamuzi wa kujiondoa kwenye mtandao huo.