Kanye West ajiingiza kwenye biashara aliyoiponda
Eric Buyanza
April 26, 2024
Share :
Rapa na mfanyabiashara bilionea wa Marekani, Kanye West ametangaza kuzindua kampuni yake ya 'ponografia'.
Miaka michache nyuma kuwaliwahi kuibuka tetesi kuwa West ana mpango wa kujiingiza kwenye biashara hiyo ya mambo ya 'watu wazima'...lakini sasa amethibitisha mwenyewe.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Kanye West aliandika: "Yeezy Porn is cumming."
Katika siku za nyuma, West aliwahi kunukuliwa akikosoa sana tasnia ya ponografia akisema hiviiii...."iliharibu familia yangu lakini Yesu ataponya kila kitu."