Kanye West atamani kutoka kimapenzi na Mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani
Joyce Shedrack
April 23, 2024
Share :
Rapa na mfanyabiashara wa mitindo kutoka nchini Marekani Kanye West akiwa kwenye mahojiano maalumu na The Download Podcast amefunguka kutamani kutoka kimapenzi na Michelle Obama Mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama.
Kanye West aliulizwa kuwa kama angepewa nafasi ya kuchagua mwanamke mwingine wa kutoka naye kimapenzi angemchagua nani ? Mwamba bila kufikiria muda mrefu akamtaja Michelle Obama.
Rapa huyo ambaye bado yupo kwenye ndoa na mwanadada Bianca Censori ambaye amekuwa akizua gumzo mitandao kwa aina ya mavazi anayovaa yanayoacha sehemu kubwa ya mwili wake kuwa wazi.
January mwaka jana walifunga ndoa yao ikiwa ni mwezi moja tu tangu West kutalikiana na aliyekuwa mke wake wa awali Kim Kardashian.