Kardinali Rugambwa na Papa Leo meza moja Vatican
Sisti Herman
June 28, 2026
Share :

Katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Makardinali unaoendelea Vatican, Baba Mtakatifu Papa Leo XIV alionekana akiwa ameketi katika meza moja na Kardinali Protase Rugambwa wa Tanzania wakati wa majadiliano ya vikundi.
Uwepo wa Kardinali Rugambwa karibu na Baba Mtakatifu unaonyesha ushiriki wake katika mijadala muhimu kuhusu maisha na utume wa Kanisa, huku Makardinali kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakishauriana kuhusu kuimarisha umoja, ushirika na mwelekeo wa Kanisa katika nyakati za sasa.





