Karia atinga mazoezini Simba ikijiandaa kuivaa Al Ahly
Sisti Herman
March 28, 2024
Share :
Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Wallace Karia jana usiku ametembelea mazoezi ya kikosi cha Simba na kuzungumza na wachezaji kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Ijumaa hii.