pmbet

Kariakoo dabi kuamua Ubingwa wa Simba Queens

Sisti Herman

April 25, 2024
Share :

Kuelekea mchezo wa dabi ya Kariakoo leo dhidi ya watani zao Yanga Princess, Kocha msaidizi wa Simba Queens Mussa Hassan 'Mgosi' amesema kuwa wanautazama mchezo huo kama 'kete' muhimu ya ubingwa kwao msimu huu, endapo kama watashinda watausogelea ubingwa zaidi.

"Maandalizi yote yapo tayari kwaajili ya kuwapa furaha mashabiki wetu wa maana ya kumaliza mchezo tukiwa na ushindi kwani malengo yetu ni kutwaa ubingwa msimu huu" alisema Mgosi kwenye mkutano na wanahabari jana.

Yanga waliopo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 21 wanawakaribisha Simba wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 31, Yanga wakiwa na mchezo mmoja wa akiba.

Je nani ataibuka mshindi? ni leo saa 10 jioni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet