Kariakoo Derby yasogezwa mbele
Sisti Herman
November 17, 2025
Share :

Bodi ya ligi kuu Tanzania imefanya mabadiliko ya ratiba ya mechi za ligi kuu Tanzania bara huku mchezo maarufu wa dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga wa mechi za mzunguko wa kwanza ukisogezwa mbele kuchezwa.
Mchezo huo uliopangwa kuchezwa Disemba 13 mwaka huu umesogezwa mbele hadi Machi mosi mwakani huku ule wa mzunguko wa pili ukichezwa May 3 2026
Mabadiliko haya yanatokana na sababu mbalimbali ikiwemo matukio ya kitaifa, mechi kimaitaifa.





