KASI YA AJABU UJERUMANI: Olise atangazwa mchezaji bora wa mwezi
Eric Buyanza
October 19, 2026
Share :

Kasi ya kutisha ya winga wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise, nchini Ujerumani imeendelea kutisha baada ya kutangazwa na kukabidhiwa rasmi tuzo ya mchezaji Bora wa Mwezi Septemba 2026, wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, anayekipiga na klabu ya FC Bayern Munich, amepokea tuzo hiyo leo tarehe 19 Oktoba 2026, ikiwa ni mwendelezo wa kiwango chake tangu ajiunge na miamba hiyo ya Bavaria.
Olise ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha uwezo wa juu sana katika mechi tatu alizocheza Bundesliga mwezi Septemba. Katika michezo hiyo, alifanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao.
Kivutio kikubwa zaidi kilikuwa kwenye mechi dhidi ya 1. FC Union Berlin, ambapo Bayern ilishinda kwa mabao 7-0 huku Olise akipiga hat-trick yake ya kwanza tangu atue Ujerumani, sambamba na kumtengenezea bao mshambuliaji tegemeo Harry Kane.





