Katika maisha yangu sijawahi kutumia pesa kupata demu - A$ap Rocky
Eric Buyanza
April 1, 2024
Share :
Rapa A$AP Rocky ambaye ni mpenzi wa mwamuziki maarufu duniani Rihanna, amejigamba kuwa katika maisha yake hajawahi kutumia pesa kupata mwanamke.
Rapa huyo ameongea hayo hivi majuzi kwenye mahojiano na mwanahabari Angie Martnez.
"Naweza kusema kwa uaminifu kabisa, katika maisha yangu sijawahi kutumia pesa kwa ajili ya kupata mwanamke".....Mimi ni Handsome hiyo inatosha" alisema.
A$AP Rocky alithibitisha uhusiano wake na Rihanna kwa mara ya kwanza katika mahojiano na gazeti la GQ mwaka 2021.
Wapenzi hao walimkaribisha mtoto wao wa kwanza wa kiume anayeitwa RZA, May 2022 na Agosti 2023, walimkaribisha mtoto wao wa pili anayeitwa Riot Ross.