Katika nchi zote za CECAFA ni sisi tu!
Eric Buyanza
December 7, 2023
Share :
Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” imewasili ikitokea Togo kwenye mchezo wa marudiano kufuzu WAFCON ambako ilifanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Morocco 2024.
Mapokezi hayo yameongozwa na Waziri wa Utamaduni, sanaa na michezo Dk. Damas Ndumbaro pamoja na Makamu mwenyekiti wa kwanza wa shirikisho la soka nchini (TFF) Athumani Nyamlani.
"Tumekuja kwa niaba ya serikali kuwapokea mashujaa wetu kwa ushindi mkubwa waliotupatia, tukumbuke katika nchi zote za CECAFA ni timu hii peke yake ndiyo imefuzu kwa wanawake, ni jambo kubwa ambalo linaleta heshima kwa nchi yetu ndani ya Afrika" alinukuliwa Ndumbaro kwenye mapokezi hayo.