pmbet

Kauli hii yazua utata; 'Mimi ndiye Baba wa muziki wa Nigeria' - Burna Boy

Eric Buyanza

May 21, 2024
Share :

Kutoka Nigeria, nyota wa muziki wa AfroBeat, Damini Ogulu (Burna Boy), amezua mjadala nchini humo miongoni wa wapenzi wa muziki na kwenye mitandao ya kijamii  kuhusu nani haswa anastahili kuwa 'Baba wa muziki wa Nigeria' baada ya msanii huyo kukitibua kwa mara nyingine tena.

Hilo limejidhihirisha kwenye tambo zake ndani ya remix mpya ya wimbo maarufu wa Afrika Kusini uitwao ‘Tshwala Bam’ wa msanii TitoM na Yuppe.

Kwenye moja ya mashairi ya wimbo huo alioshirikishwa amesikika Burna Boy akijisifu  kuwa yeye ndiye 'Baba la muziki wa Nigeria' na hivyo kuzua minong'ono kwa mashabiki wa upande wa pili (wapinzani wake kwenye muziki).

Burna Boy aliwahi kuzua mzozo kama huo miaka kadhaa nyuma baada ya kujitangaza hadharani kuwa yeye ndiye "Kioo” cha muziki wa Nigeria, hii ilikuja baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo maarufu duniani za 'Grammy'.

Mpinzani wake mkubwa Davido naye pia siku za nyuma aliwahi kujitangazia Ufalme wa muziki huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet