Kelvin John ajiunga na timu ya ligi kuu Denmark
Sisti Herman
May 31, 2024
Share :
Mshambuliaji kinda wa timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' Kelvin John amejiunga na timu ya Aalborg FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark.
Kelvin aliyekuwa na kikosi cha KRC Genk ya Ubelgiji amejiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa miaka minne.
Nyota huyo yuko nchini Denmark kwa ajili ya kukamilisha usajili huo na kufanya akosekane katika kambi ya timu ya Taifa Stars iliyoko nchini Indonesia kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.