Kendrick Lamar avuinja rekodi ya Jay Z tuzo za Grammy.
Joyce Shedrack
February 2, 2026
Share :
Rapa maarufu wa Marekani Kendrick Lamar ameshinda tuzo zote nne katika vipengele vya rap kwenye Tuzo za Grammy za 68 zilizofanyika usiku wa jana tarehe 1 februari na kuvunja rekodi ya Jay Z ya kuwa rapa wa kwanza kushinda tuzo nyingi.
Lamar anakuwa rapa wa kwanza kushinda rekodi ya mwaka mara mbili, na msanii wa kwanza wa kiume pamoja na rapa wa kwanza kushinda tuzo hiyo mfululizo. Kwa jumla, Kendrick Lamar sasa ana tuzo 27 za Grammy na hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Jay-Z, aliyekuwa na tuzo 25.
Hata hivyo mwaka uliopita 2025, alifagia tuzo kubwa kupitia wimbo wake maarufu wa “Not Like Us” ulioshinda tuzo tano, zikiwemo Rekodi ya Mwaka na Wimbo wa Mwaka.





