Kendrick Lamar avunja rekodi ya Spotify na kuweka Historia
Eric Buyanza
February 12, 2025
Share :
Rapa wa Marekani, Kendrick Lamar amevunja rekodi na kuweka historia ya kuwa rapa mwenye wasikilizaji wengi wa kila mwezi katika historia ya mtandao wa Spotify.
Wasikilizaji wa wimbo ‘Not Like Us’ kwenye mtandao wa Spotify walipanda hadi kufikia Milioni 88.8 siku ya Jumapili alipotumbuiza kwenye onyesho la Super Bowl ambalo nalo limeweka historia kwa kufuatiliwa na watazamaji milioni 133.
Kendrick amevunja rekodi ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na Drake.