KENGELE YA HATARI: Papa ataka teknolojia ya AI idhibitiwe
Eric Buyanza
September 26, 2026
Share :
Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa 14 ametoa wito kwa wataalamu wa teknolojia ya akili mnemba na viongozi wa kisiasa duniani kuwajibika kusimamia na kudhidhiti teknolojia ya AI, ili kuipunguza kasi isiuangamize ubinadamu. Na kutahadharisha kuhusu kile alichokiita "Pepo ya ulimwengu wa mashine" akitoa msisitizo kwamba kushamiri kwa teknolojia ya kisasa ya akili mnemba kunatishia kuuhujumu ubinadamu.
Papa ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya siku nne nchini Ufaransa, ikiwa ni ziara ya kwanza rasmi ya Kiserikali kufanywa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki jijini Paris tangu mwaka 2008.






