Kengold Mabingwa wa Ligi daraja la kwanza, Pamba wapanda daraja
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Ligi daraja la kwanza Tanzania (Championship) imefika tamati leo ambapo klabu ya Kengold ya mkoani Mbeya imeibuka mabingwa wa ligi hiyo baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania na kufanikiwa kufikisha alama 70 ikiwa ni wiki moja tu baada ya kufikisha alama za kupanda daraja Ligi kuu Tanzania mapema wiki iliyopita.
Pia klabu ya Pamba jiji ya Mwanza imefanikiwa kurejea ligi kuu Tanzania baada ya leo kuibuka na ushindi wa 3-1 ugenini kwa klabu ya Mbuni na kufanikiwa kujiahakikishia nafasi ya pili ambayo huwapa tiketi ya moja kwa moja timu mbili za juu kwenye msimamo wa Championship kupanda daraja moja kwa moja.
Wakati huohuo, klabu za Mbeya kwanza na Biashara United zilizojihakikishia nafasi ya 3 na ya 4 kwenye msimamo wa championship zitacheza mchujo wa mtoano wao kwa wao kabla ya mshindi baina yao kukutana na mshindi kati ya timu utakayoshika nafasi ya 14 na 15 kwenye ligi kuu (Play-offs).
Timu za Pan African na Ruvushooting zimeshuka daraja la kwanza hadi la pili baada ya kushika nafasi mbili za mwisho.