Kenya kuacha kuagiza viatu kutoka nje - Ruto
Eric Buyanza
June 3, 2024
Share :
Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza serikali yake itawekeza mamilioni ya fedha katika kiwanda cha kutengeneza viatu, na ifikapo mwaka 2027 Kenya itakoma kuagiza viatu kutoka nje.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Madaraka Day, Ruto alisema kiwanda hicho kitachangia ongezeko la uzalishaji viatu jozi milioni nane hadi jozi 36 milioni kwa mwaka.
“Hii itahakikisha kuwa taifa letu linajitosheleza kwa viatu kiasi kwamba ifikapo mwaka wa 2027 tutakoma kuagiza viatu kutoka nje”
“Narudia hapa kwamba baada ya kiwanda hicho kuanza kazi, hatutakuwa tukiagiza viatu kutoka ng’ambo. Tutakuwa tukivalia viatu vyetu, vilivyotengezwa nchini Kenya kwa kutumia ngozi yetu,” Dk Ruto akasisitiza.