pmbet

Kenya kustaafisha ndege pekee ya Rais 2026

Sisti Herman

September 18, 2025
Share :

 

Kenya inatarajia kustaafisha ndege pekee ya rais aina ya Fokker 70 ifikapo mwaka 2026, kufuatia changamoto za mara kwa mara za kiufundi na gharama kubwa za matengenezo ya ndege hiyo.

Katika mahojiano na gazeti la @nation , Waziri wa Ulinzi nchini Kenya, Soipan Tuya, amethibitisha kuwa ndege hiyo, yenye miaka 30 , ilisafirishwa Agosti 22 hadi katika kiwanda cha Fokker Techniek kilichopo Woensdrecht, Netherland, kwa ajili ya ukarabati wa mwisho unaotarajiwa kuchukua mwaka mmoja.

Baada ya kurejea Kenya, ndege hiyo itatumika kwa muda mfupi kisha kuondolewa rasmi kwenye huduma, kufuatia mapendekezo ya Fokker Techniek kuwa ndege hiyo haifai kuendelea kutumika zaidi kutokana na uhaba wa vipuri na gharama kubwa za uendeshaji wake.

Foker 70 yenye namba ya usajili KAF308, maarufu kama Harambee One, imekuwa ikihudumia safari za marais wa Kenya tangu iliponunuliwa ikiwa mpya.

Waziri Tuya amesema kuwa ununuzi wa ndege mpya ya rais unaweza kufanyika ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo endapo bajeti itaruhusu, ingawa maelezo zaidi hayajafichuliwa.

Kwa sasa, Rais Ruto atalazimika kutegemea ndege za Jeshi , ndege za abiria za Kenya Airways, au ndege za kukodi kwa ajili ya safari rasmi.

Katika ziara yake ya hivi karibuni, kati ya Septemba 7 hadi 9, kuelekea Mkutano wa Pili wa Hali ya Hewa Afrika nchini Ethiopia, Rais Ruto alitumia ndege aina ya Gulfstream GV inayomilikiwa na kampuni ya Skymark Executive ya Dubai, ambayo imekuwa ikihudumu jijini Nairobi tangu Oktoba 2024.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet