pmbet

Kenya yaondoa kodi kwenye mkate kufuatia maandamano

Eric Buyanza

June 19, 2024
Share :

Serikali ya Kenya imefutilia mbali mipango ya kuongeza tozo kwenye mkate, magari na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na kuufanyia marekebisho muswada wenye utata ambao umechochea maandamano nchini humo.
 

Ofisi ya Rais imesema imeondoa pia tozo mpya kwenye miamala ya simu, usafirishaji wa sukari na mafuta ya mboga.
Wabunge walitarajiwa jana kuujadili muswada huo mpya wa fedha japo mjadala huo umeahirishwa hadi leo, saa chache tu kabla ya ofisi ya rais kutangaza mabadiliko hayo.
 

Taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki limekabiliwa na mzozo juu ya kupanda kwa gharama ya maisha huku wakosoaji wakionya kuwa tozo hizo mpya zitawaongezea Wakenya mzigo mkubwa zaidi.
 

Mamia ya waandamanaji wengi wao wakiwa vijana walikusanyika karibu na bunge kupinga tozo hizo mpya huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya. Shirika la kutetea haki za binadamu la KNHCR limesema watu 335 wamekamatwa.

VOA

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet