Kenya yatangaza Mei 10 siku ya mapumziko kuwakumbuka wahanga wa mafuriko
Eric Buyanza
May 9, 2024
Share :
Serikali ya Kenya imetangaza siku ya Ijumaa (Mei 10) kuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko.
Rais wa Kenya William Ruto amesema amesema siku hiyo itatumika kukumbuka maisha ya Wakenya walioathirika na walioaga dunia kutokana na mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Siku hiyo pia imetengwa kwa ajili ya zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.