Kepa aibuka shujaa Arsenal ikitinga nusu fainali Carabao Cup.
Joyce Shedrack
December 24, 2025
Share :
Kipa wa Arsenal, Kepa Arrizabalaga, alikuwa shujaa asiyetarajiwa Jumanne usiku, huku washika bunduki hao wakiisambaratisha Crystal Palace na kuingia nusu fainali ya Kombe la Carabao baada ya mikwaju ya penalti.
Vijana hao wa London Kaskazini walitangulia kwa bao la kujifunga la Maxence Lacroix lakini dakika za mwisho Marc Guehi aliisawazishia
Crystal Palace.
Mchezo uliisha 1-1 kisha ukawa wa mikwaju ya penalti huku Kepa akiokoa shuti la Lacroix na Arsenal ikishinda 8-7 ya mikwaju na kutinga nusu fainali ambapo watakutana na Chelsea.
Baadhi ya mikwaju ya penati ya Arsenal iliwekwa kimiani na Odegaard, Declan Rice, Saka, Trossard na Mikel Merino.





