pmbet

Kepa Arrizabalaga kuchukua mikoba ya David Raya

Eric Buyanza

June 6, 2025
Share :

Arsenal wameanza mazungumzo ya kumsajili mlinda mlango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga kama mbadala wa David Raya. 

The Gunners wanahitaji kipa wa pili baada ya mkopo wa Neto kutoka Bournemouth kuisha na klabu hiyo kushindwa kumsajili Joan García wa Espanyol, ambaye anajiunga na Barcelona. 

Kepa alitumia msimu uliopita kwa mkopo huko Bournemouth na hana mustakabali ndani ya Chelsea, licha ya The Blues kutumia pauni milioni 71.6 kumsajili kutoka Athletic Club mwaka 2018 (rekodi ya dunia kwa golikipa). 

Sasa anaweza kusajiliwa kwa pauni milioni 5 tu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet