Kesi kumsesha Diddy tuzo za Grammy
Sisti Herman
January 15, 2024
Share :
Rapa maarufu kutoka nchini Marekani P. Diddy hatoshiriki katika Tuzo za Grammy mwaka 2024 kufuatia na kesi nyingi zinazo mkabili licha ya kuteuliwa kuwania tuzo katika kinyang’anyiro hicho.
2023 ni mwaka mbaya kwa Diddy ambapo alikabiliwa na kesi kadhaa za unyanyasaji wa kingono na makosa mwengine ya ulaghai anayotuhumiwa k kuwahi kuyafanya miaka ya nyuma.
Ikumbukwe kuwa Diddy aliteuliwa kuwania Tuzo katika kipengele cha Album bora ya R&B kupitia album yake ya ‘The Love: Off the Grid’.