Kesi ya Chris Brown na Abe Diaw yazimwa nje ya Mahakama.
Joyce Shedrack
July 1, 2025
Share :
Taarifa zinasema kuwa , Chris Brown Ameripotiwa Kufikia makubaliano katika kesi iliyofunguliwa na mtayarishaji ‘Abe Diaw’, ambaye alimtuhumu kwa kumpiga na chupa katika klabu moja huko London mwaka 2023.
Diaw alidai kuwa Breezy alimpiga mara 3 na chupa ya Don Julio ya 1942 hadi kupoteza fahamu kipigo kilichosababisha kupata mejaraha ya muda mrefu.
Ijumaa iliyopita Diaw aliwasilisha ombi kwa Jaji wa Los Angeles kuitupilia mbali kesi hiyo, ‘Prejudice’ yani hatoweza kuifungua Tena.
Hii inaonesha kuwa wawili hawa wamemalizana chini kwa chini nje ya Mahakama.
Hata hivyo hakuna kati yao aliyeibuka Kusema chochote juu ya msala huo au kama walimalizana kwa njia ya kulipana fedha.