Kesi ya Gekul yafutwa
Eric Buyanza
December 27, 2023
Share :
Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imeifuta kesi iliiyokuwa ikimkabili mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul kuhusiana na tuhuma za kumshambulia aliyekuwa mfanyakazi wake, Hashim Ally.
Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Victor Kimario baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo na ameiondoa kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 ambayo inampa DPP Mamlaka ya kuondoa kesi yoyote ya jinai Mahakamani kabla haijafikia hukumu.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Hashim kupitia kwa wakili Peter Madeleka ambaye amesema wanakusudia kukata rufaa kwakuwa hawajaridhishwa na maamuzi ya mahakama.